| Mbio pekee inayochukua wakimbiaji wengi zaidi ni Vodacom 5km fun run na safari hii mbio hizi zilianzia jirani kabisa na Zumba . |
| Wadada wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,MUWSA pia walikuwepo katika mbioz hizo. |
| Wenye ulemavu pia walishiriki vyema kabisa. |
| Hatimaye wakahitimisha mbio katika uwanja wa Ushirika. |
| Kuna wakimbiaji wengine walitiliwa shaka kama ni washiriki ama walaikuwa na kazi nyingine kama huyu aliyekuwa akihitimisha mbio za Km 42 bila ya kuwa na namba ya ushiriki. |
| Huyu nae alihitimisha mbio kwa kuchechemea. |
| Mshiriki huyu sasa yeye alikuwa anahitimisha mbio za Km 21 akiwa amebeba mfuko uliokuwa na vitambaa vya kufunga kichwani ,swali je alikimbia huku akiendelea na biashara kwa wakimbiaji? |
| Hapa sasa,huyu jamaa alilzimika kuhitimisha mbio akiwa peke yake maana kila mkimbiaji aliyemsogelea alionekna kutokuwa na imani nae. |
| Huyu alichomoka Tuition akaamua na yeye kuhitimisha mbio akiwa na madaftari yake. |
| Wazee wa viatu vya matairi pia walikuwepo kutoa burudani. |
| Baada ya kujaa upepo kwa muda mrefu Puto hili lianza kuanguka taratibu ili kutoa nafasi kwa wapiga picha waweze kupiga kilele cha mlima Kilimanjaro kwa ufasaha. |
| Hatimaye likatoa shughuli nyingine kwa watu waliokuwa na kazi ya kurekodi wakimbiaji. |
| Wakimbiaji walihitimisha mbio kwa kuinama. |